Tunafungua milango ya siku zijazo! ๐จโ๐ซ Tulifanya mhadhara katika Chuo cha Uhasibu Tanzania, mada kuu ikiwa ni juu ya udahili wa wanafunzi kwenda kusoma nchini Urusi, kwa ufadhili wa serikali ya Urusi. Wanafunzi wakafahamu juu ya fursa na uwezekano wa kupata elimu ya juu katika vyuo vikuu vya Urusi. Tuliwaeleza kwa kina: โ kuhusu utaratibu wa kuwasilisha maombi; โ kuhusu nyaraka muhimu zinazohitajika; โ kuhusu manufaa ya kusoma nchini Urusi, na pia juu ya maisha ya mwanafunzi awapo nchini humo. Je, unataka pia kwenda kusoma nchini Urusi, kwa ufadhili? Taarifa zote, na pia maelekezo muhimu yataweza kupatikana katika Maonyesho yetu ya Elimu ๐ Jumatatu, Novemba 9 โฐ Saa 4:00 asubuhi ๐ Kituo cha Sayansi na Utamaduni cha Urusi, jijini Dar Es Salaam Jisadili kwenye mtandao huu: https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSd7GjXtjpmDDM-IUMqz6hQX_49bus4NgD9e8nngZ-HZF_4FlQ/viewform