Hivi umewahi kwenda kwenye ukumbi wa starehe mbako machungwa hugawiwa kwa watazamaji wakati wa onyesho? ๐๐๏ธ Hivi ndivyo marafiki zetu, waigizaji wa Kikundi cha Sanaa za Maigizo โAFASRโ, walivyofanya kwenye tamasha kule Bagamoyo. waliigiza igizo, "Kabaila Hayawani" ๐ Ila, waigizaji wa Kikundi hiki waliwezaje kusoma fasihi ya Kirusi? Sisi, Jumba la Urusi Dar Es Salaam, tulitafsiri kazi hiyo kwa Kiswahili. Huwa tunafanya hivi kila mwaka - tunatafsiri hadithi za waandishi maarufu wa Urusi, tunachapisha vitabu na kuvitoa zawadi kwa Maktaba ya Taifa ya Tanzania. ๐ญ Katika Tamasha la 44 la Kimataifa la Sanaa lililofanyika Bagamoyo, igizo la "Kabaila Hayawani" lilifana sana! Watazamaji walijikuta wakishiriki pia - walifanya biashara na waigizaji "sokoni", pale pale ukumbini, na pia wakashiriki katika baraza la kijamii juu ya kesi dhidi ya "Kabaila Hayawani", walistushwa na kumuogopa dubu wa Kirusi alipotokea, ila walifurahishwa sana na jinsi haki ilivyotendeka katika hitimisho la shauri hilo.