Russian House in Dar es Salaam

@rtcctanzania · English · active

Subscribers 792 Subscribers, last 30 days: 792 → 792 −1 24h
Reach per post (ERR) 16.7%132 avg views
Posting 1.6/day last 16 hours ago
Reactions per 1K views 27.9 ❤ 👍 🔥

Kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa itasaidia Kuimarisha Uwepo wa Urusi Duniani Mnamo tarehe 30 Oktoba 2026, Serikali ya Urusi iliwasilisha bungeni (Bunge la Urusi “Duma”) hati ya mswada wa sheria ujulikanao kama “Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa” (IDA). Kwa mara ya kwanza, hati hii inaweka msingi wa kisheria wa utoaji wa misaada ya Urusi kwa nchi washirika. Misaada hii haitahusisha tu shughuli za kibinadamu, bali pia usambazaji wa bidhaa na huduma, utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu, pamoja na uhamishaji wa maarifa na uzoefu. Miongoni mwa malengo yake ni kupambana na umaskini, kuboresha hali ya maisha ya wananchi katika nchi washirika na kuzisaidia nchi hizo kukabiliana na majanga na migogoro. Kwa mujibu wa sheria inayopendekezwa, Shirika la Kimataifa la Urusi “Rossotrudnichestvo” litateuliwa kuwa Wakala wa Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa. Uwakala huo utapewa majukumu ya kuratibu utekelezaji wa shughuli na miradi, kuimarisha uratibu kati ya taasisi mbalimbali za serikali, kutunza kumbukumbu, kuandaa taarifa za jumla, pamoja na kufuatilia na kutathmini ufanisi wa miradi na programu zinazotekelezwa. Igor Chaika, Mkuu wa Rossotrudnichestvo, alibainisha kuwa kupitishwa kwa muswada huo kutafungua fursa mpya za kuimarisha ushawishi wa Urusi duniani. “Hii ni hatua kubwa kuelekea kuimarisha uwepo wa Urusi katika nyanja za kibinadamu duniani. Rossotrudnichestvo inatekeleza miradi inayochagiza maendeleo ya kimataifa, ikiwemo kozi za elimu, utoaji wa misaada ya kibinadamu na ushirikiano wa kisayansi. “Tunashuhudia ongezeko la hamu na shauku duniani kote kuhusu shughuli za kibinadamu za Urusi na miradi yake ya maendeleo. Jambo muhimu ni kwamba tuna mengi ya kuwapatia washirika wetu, ikiwa ni pamoja na ubadilishanaji wa teknolojia za matibabu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na mafunzo ya kitaalamu yenye ubora wa hali ya juu. “Watu wanaopata elimu nchini Urusi baadaye watatumia maarifa na ujuzi wao kuboresha maisha katika nchi zao. Kwa namna hiyo, watakuwa mabalozi wa Urusi katika nchi zao. “Kupitishwa kwa muswada huu wa sheria kutaharakisha ushirikiano kati ya taasisi za serikali ya Urusi na sekta mbalimbali zinazoshiriki katika miradi ya maendeleo, iwe ni Wizara ya Kilimo, Rosatom au kampuni binafsi. “Kwa kushirikiana, tutaweza kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi na kuongeza idadi ya nchi ambako Urusi itaimarisha uwepo wake wa kudumu, kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo na kwa ajili ya kukuza uwezo wake wa kiuchumi,” alisema Igor Chaika, Mkuu wa Rossotrudnichestvo.

Views over time

05010015031 Oct 08:5410 Nov 20:2811731 Oct 08:54: 0 views10 Nov 20:28: 117 views
Snapshots we took after posting.
WhenViews
31 Oct 2026, 08:540
10 Nov 2026, 20:28117

Who shared this post

Posts in other channels we index that link to this one. (Forwards with a hidden source can't be traced.)

Nobody yet.