🤝 Naibu Mkuu wa Rossotrudnichestvo kwenye kongamano la “Urusi —Afrika”: Tutafanya kila kinachowezekana ili nchi za Afrika ziweze kujisikia huru kabisa na ziweze kukuza ushirikiano wa kibinadamu na Urusi 📌 Mahusiano kati ya Usovieti na Afrika yalijngwa kwa vitendo halisi, na matokeo yake yangali bado yanaonekana katika bara hilo hadi leo. Hayo yamesemwa na Konstantin Kolpakov, Naibu Mkuu wa Rossotrudnichestvo, katika kikao cha jopo " Historia ya Chaguo la Pamoja: Mahusiano kati ya Usovieti na Afrika, katika Kumbukumbu ya Bara hilo, na Siasa za Leo," ambayo lilifanyika katika uwanda wa Tatu wa uchumi na huduma za kijamii waKongamano la “Urusi —Afrika”. "Jukumu letu ni kuutimliza urithi huu wa kihistoria kwa mshiko mapya,tukigeuza kuaminiana kulikojengwa katika msingi imara wa ushirikiano," alisema. "Tutafanya kila kitu ili kuzifanya nchi za Afrika zijisikie huru na ziweze kuendeleza ushirikiano wa kibinadamu na Urusi." ➡️ Kulingana na yeye, mfano halisi wa mwingiliano kama huo ni mradi wa Ofisi ya ossotrudnichestvo kwenye stendi ya pamoja na ANO Eurasia kule “Gostiny Dvor.” Kila mhudhuriaji anaweza kutoa wazo lake, ambapo likiwa na ubora ustahilio, atapata ufadhili kupitia mfumo wa “Ruzuku ndogondogo”, ambao utazinduliwa na Uwakala huo utazindua mnamo mwaka 2027. 🌍 Kama alivyosema, Rossotrudnichestvo inaendelea kuongeza uwepo wake Barani Afrika - Majumba 25 Urusi yameongezwa kwenye idadi ya Majumba tisa yalizopo, ambayo yako Burkina Faso, Ghana, Guinea, Kenya, Nigeria, Senegal na nchi zingine. Kuna ofisi rasmi za Uwakilishi Nchini Misri (Kairo na Aleksandria), Zambia, Moroko, Jamhuri ya Kongo, Tanzania, Tunisia na Ethiopia. Wafanyakazi wengine wawili wanafanya kazi katika balozi za Urusi Nchini Afrika Kusini na Angola, ambapo kunafanyika maandalizi mahsusi kwa ufunguzi rasmi wa Jumba la Urusi jijini Luanda. Makubaliano na Aljeria, Mali na Gine hivi sasa yanajadiliwa. "Lugha ya Kirusi si tu lugha ya utamaduni-tajiri na urithi, bali pia ni lugha ya siku zijazo, lugha ya mafanikio. Ni lugha ambayo kwayo wavulana na wasichana wa Kiafrika wanaweza kujitambua. Kuifundisha, ni moja ya malengo ya Majumba ya Urusi," Konstantin Kolpakov alisisitiza. ❗️ Naibu Mkuu Wa Rossotrudnichestvo aliongeza Kuwa, Shirika hilo ni muwezeshaji mkuu wa hatua za mwanzo za udahili wa vijana wa kigeni kwenda kusoma nchini Urusi, kwa ufadhili wa serikali. Zaidi ya nafasi 5,300 zimetengwa kwa ajili ya nchi za Afrika katika mwaka wa masomo wa 2025/2026, na ufadhili umeongezeka katika mwaka huu mpya wa masomo, Na Chad, Angola, Algeria, Misri na Mali ni wanufaika wakubwa. Idadi ya washiriki wa Kiafrika katika Mpango wa ziara za Muda mfupi za “Kizazi Kipya” kwenda Urusi, imeongezeka zaidi ya mara mbili katika mwaka uliopita. Kwa kuongezea, alitangaza kusainiwa kwa mkataba kati ya Krasnodar na Antsirabe (Madagaska). Rejista ya jumla ya makubaliano kati ya manispaa sasa itajumuisha makubaliano 28 na miji ya Afrika. 📅 Kongamano hilo linafanyika Mosko mwezi huu wa Oktoba (tarehe 28-29), na limeleta pamoja zaidi ya makundi 48 ya wawakilishi kutoka nchi 54 za Afrika, kati yao 22 wakiwa ni wakuu wa nchi. Programu ya mijadala inajumuisha vikao vyenye zaidi ya mada 40 na majadiliano ya kijopo, ambapo kutakuwa na wanenaji wapatao 100.
Russian House in Dar es Salaam
Subscribers
792
−1 24h
Reach per post (ERR)
16.7%132 avg views
Posting
1.6/day
last 16 hours ago
Reactions per 1K views
27.9
❤ 👍 🔥
Views over time
| When | Views |
|---|---|
| 29 Oct 2026, 15:11 | 0 |
| 10 Nov 2026, 20:28 | 126 |
Who shared this post
Posts in other channels we index that link to this one. (Forwards with a hidden source can't be traced.)
Nobody yet.